CHUO CHA
UALIMU MURUTUNGURU
Tel.No:+255752416009 S.L.P
68
Mail:murutungurutc.@gmail.com NANSIO
Website:http/www.moe.go.tz UKEREWE-MWANZA
Ndugu............................................................
MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA
ASTASHAHADA YA ELIMU YA MSINGI NA ELIMU YA AWALI MWAKA WA MASOMO 2019/2020
Kwa
niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ninapenda kukupongeza kwa
kuchaguliwa kwako kujiunga na Astashahada ya Elimu ya Msingi / Astashahada ya
Elimu ya Awali katika chuo cha ualimu Murutunguru kwa mwaka wa masomo
2019/2020. Mafunzo yatakuwa ya miaka miwili tu.
Yafuatayo
ni maelekezo muhimu, yasome kwa makini na kuyazingatia.
- KUFUNGUA CHUO
Chuo kitafunguliwa tarehe 10.08.2019.Unatakiwa ufike chuoni
bila kukosa kuanzia tarehe 10.08.2019 hadi tarehe 24.08.2019 bila kukosa. Baada
ya hapo hautapokelewa kabisa na nafasi yako atapewa mtu mwingine.
- MAHALI CHUO KILIPO
Chuo cha ualimu Murutunguru kipo katika wilaya ya Ukerewe
mkoa wa Mwanza.Kipo umbali wa km 13 kutoka Nansio mjini ambako ndiko makao
makuu ya wilaya ya Ukerewe.
Unaweza kuingia Ukerewe mpaka chuoni kwa njia zifuatazo:-
i.
Kwa magari (basi) kutoka
Bunda hadi Nansio.
ii.
Kwa meli kutoka Mwanza
hadi Nansio. Usafiri upo kila siku kwa njia zote mbili
.
- VIFAA VYA KUJA NAVYO CHUONI
- MAVAZI
i.
Sare za chuo
Wavulana: Njoo na:-
●
Shati mbili: nyeupe moja
(1) na light blue moja (1), zote
mikono mirefu (tetron).
●
Suruali mbili (2) nyeusi
zisizo na marinda na zisiwe za kubana.
●
Koti moja (1) jeusi
lenye kitambaa sawa na suruali na
mipasuo miwili nyuma.
●
Jozi mbili (2) za viatu
vyeusi (ngozi).
●
Tai mbili (2) nyeusi.
●
Soksi nyeusi jozi mbili.
Wasichana: Njoo
na:-
●
Shati mbili (2): nyeupe
moja (1) na light blue moja (1) zote
mikono mirefu (tetron).
●
Sketi mbili (2) zote
rangi nyeusi (za heshima); nusu solo
ivuke magoti na isiwe na marinda.
●
Jozi mbili (2) za viatu
vyeusi (soli fupi).
●
Koti moja (1) jeusi
lenye kitambaa sawa na sketi.
●
Tai moja (1) fupi rangi
nyeusi.
●
Juba mbili (2) nyeupe
moja (1) na light blue moja (1) kwa
waislamu tu.
●
Soksi nyeupe jozi mbili.
- VIFAA VYA MICHEZO
Wavulana: Njoo na:-
●
Jezi jozi moja (1) ya
michezo Taifa Stars bluu (T-shirt na bukta yake).
●
Soksi za stocking za bluu zenye fito nyeupe.
●
Raba za michezo rangi
yoyote.
●
Jozi moja (1) ya truck suit rangi ya bluu
●
Vifaa vingine vya
michezo utakavyoona vinafaa.
●
T-shirt yenye nembo ya
chuo itapatikana chuoni kwa Tshs. 15,000/=
Wasichana: Njoo na:-
●
Jezi jozi moja (1) ya
michezo ya Taifa Stars bluu (T-shirt na bukta yake).
●
Sketi moja (1) fupi
rangi yoyote.
●
Raba za michezo rangi
yoyote.
●
Jozi moja (1) ya truck
suit rangi ya bluu.
●
Vifaa vingine vya
michezo utakavyoona vinafaa.
●
T-shirt yenye nembo ya
chuo itapatikana chuoni kwa Tshs. 15,000/=
- VIFAA VYA MALAZI
Chuo kitakupatia kitanda. Hivyo njoo na
:-
●
Godoro lako futi mbili
na nusu (2.5) kwa sita (6) Au kwa watakaowahi yapo machache ya kukodi.
●
Blanketi moja (1).
●
Shuka mbili (2) light
blue zisizo na maua ya kutarizi na foronya zake.
●
Mto mmoja (1).
●
Chandarua.
- VIFAA VYA CHAKULA
Njoo na:-
●
Bakuli moja (1), sahani
moja (1), kikombe aina ya ‘mug’ na
kijiko.
- VIFAA VINGINEVYO
Njoo na ndoo moja (1) kwa ajili ya maji
ya matumizi yako binafsi na kazi nyinginezo.
- VIFAA VYA MASOMO
Fika na vifaa vifuatavyo kwa ajili ya
masomo:-
●
Madaftari ya kutosha
masomo yote.Yasipungue kumi na mawili.
●
Kalamu za wino (bluu na
/ au nyeusi tu)
●
Kalamu za risasi.
●
Mkebe wa vifaa vya
Hisabati (Mathematical Set).
●
Rula.
●
Counter
Book moja (1) Quire 3 kwa
ajili ya Mafunzo ya Ualimu kwa Vitendo.
●
Kitabu kimoja (1) cha
Elimu ya Msingi cha somo lolote chenye ithibati ya Taasisi ya Elimu Tanzania.
- MAHITAJI KWA AJILI YA USAJILI
Ili uweze
kusajiliwa lazima uje na:-
●
Vyeti vyako halisi vya
taaluma (original academic certificates) vya kuhitimu elimu ya sekondari kidato
cha nne na cha sita kama umehitimu ngazi hiyo.
●
Cheti au vyeti vyako
halisi vya kumaliza elimu ya sekondari {Leaving certificate(s)} kwa ngazi zote
za elimu ulizopitia.
●
Kitambulisho chochote
chenye picha yako kinachokutambulisha.
●
Hati ya daktari kwa
ajili ya uthibitisho wa afya yako.Na kwa wenye kadi za bima ya afya waje nazo.
●
Jarada (file) moja (1)
la kutunzia kumbukumbu zako.
●
Risiti halisi za malipo
za benki (original bank pay-in-slip) ya michango. Ada utalipia chuoni
baada ya kupatiwa control number.
●
Cheti cha kuzaliwa.
NYONGEZA:
Kwa
wale ambao vyeti vyao bado havijatolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania, njoo
na karatasi ya matokeo (result slip au
statement of results) iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
- VIFAA VINGINE UNAVYOPASWA KUWA NAVYO WAKATI WA KUSAJILIWA
Ni
pamoja na:-
●
Ream moja (1) A4 ya
karatasi nyeupe kwa ajili ya shughuli za kiofisi.
- MCHANGANUO WA MALIPO YA ADA NA MICHANGO
AINA YA
MALIPO AU KIFAA
|
KIWANGO
|
NAMBA YA AKAUNTI
|
JINA LA AKAUNTI
|
ADA
|
450,000/= kwa mwaka au 225,000/=kwa
muhula. Isilipwe hadi hapo
utakapopatiwa control number
ukisharipoti chuoni.
|
31401100005
|
MURUTUNGURU TC REVENUE
COLLECTION ACCOUNT.
|
MICHANGO
|
NB: Suala la mchango
wa mahafali litajadiliwa na wanachuo wenyewe.
|
31401100001
|
PRINCIPAL MURUTUNG-URU TTC.
|
JUMLA: 150,000/=
|
|||
NYONGEZA
Chuo
hakipokei fedha taslimu wala hundi, michango yote inatakiwa kukamilika ndipo
usajiliwe.
- SHERIA NA TARATIBU ZA CHUO
Pamoja na kukidhi vigezo
vya kusajiliwa na kuwa mwanachuo kamili, mwanachuo atatakiwa kusoma sheria,
kanuni na taratibu za chuo mara tu afikapo chuoni na hatimaye atajaza fomu ya
kukubali sheria, kanuni na taratibu hizo.
Kwa mawasiliano zaidi piga:
1. 0765
612 822 / 0784 461 659 Mwadili wa wanachuo
2. 0765
618 026 / 0745 954 401 Msajili wa wanachuo
3.
0713 356 947/ 0755 432 991Mratibu Taaluma
BALBINA L.
JOSEPH
MKUU WA
CHUO
KIAMBATISHO
A: FOMU YA KUPIMA AFYA (Ijazwe na daktari
na kugongwa muhuri)
THE
GOVERNMENT OF TANZANIA
REQUEST
FOR MEDICAL EXAMINATION
PART A:
From: Murutunguru Teacher’s college
From: Murutunguru Teacher’s college
TO: The Medical Officer
..................................................................
.................................................................
Please
examine the above named as to his/her physical and mental fitness for a full
time teacher course.
A:
1. (a) Eye- sight
(b) Hearing
(c) Speech
(d) Venereal Diseases
(e) Leprosy
(f) Limbs
(g) Epilepsy
2.
Neuroses
3. Other serious Diseases
B.
Blood Group
Date..................................
Signature................................... Official Stamp
***************************************************************************
PART B: MEDICAL
CERTIFICATE
(To be completed by Government
Medical Officer)
I
have examined the above named student that he/she is physically fit/ unfit and
mentally *fit/unfit for a full time Teacher Education course
Eye
Sight.........................................................................................................................
Hearing.................................................................................................................................
Limbs.................................................................................................................................
Speech.................................................................................................................................
Leprosy..............................................................................................................................
Neuroses............................................................................................................................
Other
serious
Diseases.........................................................................................................
Pregnancy...........................................................................................................................
Date:
...........................................................
Signature..........................................................
Official Stamp
